
KUMEKUWA na madai mazito kwamba, mama wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Mama Dangote’ amemtuliza kimapenzi mumewe, Maisara Abdul ‘Uncle Shamte’ ambaye naye amepagawa ile mbaya bila kujali tofauti za kiumri. Sasa taarifa mpya ni kwamba, mwishoni mwa wiki iliyopita, Shamte alitishia nyau kwa kumwambia Mama Dangote atamuacha, ndipo akakiona cha mtema kuni.
Tishio hilo la Shamte liliwafanya baadhi ya wafuasi wa Mama Dangote kwenye ukurasa wa Instagram kumvamia na kumtaka kuacha mara moja kuushtua moyo wa mama huyo. Kuthibitisha hilo, Mama Dangote amekuwa akisisitiza mara kwa mara; “Hakuna furaha kubwa kama kupendwa na mtu unayempenda kwa moyo wako wote.
“Kila siku nimekuwa sina namna zaidi ya kumshukuru Mungu kwa zawadi hii kubwa aliyonipa. Kwa kunipatia mwanaume sahihi wa maisha yangu. Ninampenda mno mume wangu Uncle Shamte.”

Kwa upande wake Uncle Shamte, naye amekuwa akimthibitishia Mama Dangote; “Kupendana ndiyo jadi yetu mke wangu.”Inavyoonekana, mambo yanaanza kubadilika kwenye penzi lao kiasi cha Shamte kumtishia Mama Dangote kuwa atamuacha.
Kuhusu sakata jipya ilikuwa hivi; mama Dangote aliposti video ya mjukuu wao, Tiffah Dangote kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonesha anazungumza na baba yake, Diamond ambapo Shamte, akiwa mmoja wa wafuasi wa mama huyo, aliweka maoni yake akimtaka kutoa tafsiri ya kile alichokuwa anazungumza Tiffah la sivyo atamuacha wiki hii.
Kufuatia kauli hiyo ya Uncle Shamte, ndipo wakaibuka wafuasi wakali kama pilipili wakimtaka kuacha kumpa Mama Dangote maumivu ya moyo bila sababu za msingi.
Baadhi ya wafuasi walitafsiri kauli hiyo kuwa huwenda Uncle Shamte anataka kumuacha Mama Dangote akaoe mwanamke mwingine.
Hata hivyo, baada ya mjadala kuwa mkali, Mama Dangote alirejea na kumwambia; “Uncle Shamte huwezi kuoa zaidi yangu miye, mimi ndiye kabari yao.”
Kauli hiyo iliwapooza kidogo wafuasi wake hao kwa kuona kuwa Mama Dangote anajiamini kuwa hawezi kuachwa na jamaa huyo, kwani hana ubavu wa kufanya hivyo.
Baadhi ya maoni ya wafuasi hao yalisomeka hivi;
kpazzy_official: Amtanie nani sasa kama siyo mke na wajukuu acha (tusi) basi kidogo.
alimanassor67: Uncle Shamte teamo teamo forever kwa Mama Dangote.
Zarithebossldd: Mama Dangote ha ha haaaa unakubalije Tee akutoe???? Ila acha iwe zamu ya Tee we nenda zako kwa Nillan.
mwaifwanikisa: Mama Dangote unapinduliwa Mrs Shamte. Tiffah kaja na moto haahaaa unamuogopa Tiffah kumbe ndiye kiboko yako.
fridahkendij: Mama Dangote wewe ni Tiffah and Tiffah ni wewe.
arrow_princess: Uncle Shamte mwambie mama Dangote afanye warudiane Zari hana njaa kama wa hapa Bongo wanajifanya wajinga ili wapate hela na mali, mtakosa hata misaada wakiolewa wa Bongo.
rozy2054: Mama Dangote haya, wewe umepata mke mwenza tayari…
Baada ya kuona sekeseke hilo, gazeti hili lilimtafuta Uncle Shamte ambaye alipoulizwa juu ya ishu hiyo aliishia kucheka kisha akakata simu.