×

JPM Amshangaa Ndugai Kuvaa Barakoa Bungeni – Video

RAIS John Magufuli ameleza kushangazwa kwake na spika wa Bunge, Job Ndugai, kuvaa barakoa bungeni tena akiwa ameketi kwenye kiti chake peke yake ilihali ugonjwa wa corona nchini umekwisha.

 

Amesema hayo leo Ijumaa, Juni 5, 2020 wakati akihutubia Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), jijini Dodoma na kuwataka wananchi kutokuwa na hofu kuhusu ugonjwa huo huku akiwataka kutovaa barakoa za misaada kwani hazijulikani kama zina usalama ama la!

 

“Corona imekwisha ndiyo maana hata mabarakoa hakuna, hata leo tunaonana tu hapa kawaida, ndiyo maana nilikuwa namshangaa Spika Ndugai akiwa Bungeni yupo kiti chake peke yake lakini amelivaa hilo libarakoa mdomoni, Watanzania tumtangulize Mungu.

 

“Njia nyingine ambayo inaweza kutumika ni kuletewa vifaa vya corona vyenye corona, anapokuletea mtu barakoa hujui ameitoa wapi kataa, mwambie kavae wewe na mke wako na watoto wako nyumbani…

 

“Ukitaka kuvaa barakoa kashone yako, mbona ni rahisi tu, barakoa mbona imekaa kama titi moja la mtu mmoja hivi limekatwa upande mmoja, weka huku kama… aaah samahani mheshimiwa waziri nimesema hapa, nilikuwa nachomekea tu kidogo,” amesema.

Leave a Comment