×

Johari: Wasanii wa Sasa Wanakurupuka

MSANII mkongwe kwenye tasnia ya filamu nchini, Johari Chagula ”Johari”, amefunguka kuwa wasanii wa sasa hivi hawafanyi kazi kwa weledi bali wanafanya kazi kwa kukurupuka.

 

Akizungumza na  Amani Johari amesema kuwa katikasanaa ya zamani wasanii walikuwa lazima waingie kwenye mafunzo ya kuigiza lakini  ni kwa sasa  imekuwa tofauti yaani kila mtu amekuwa msanii.

 

“Kwenye mambo ya  uigizaji kuna mambo mengi sana yamebadilika kwa sababu sanaa ya zamani ilikuwa ni sanaa ya mapokezi,  kwa hiyo kile tulichokuwa tukikifanya watu wanakipokea kwa mashamsham kwa sababu kilikuwa na mafuzo ndani yake  lakini sanaa ya sasa imebadilika kwa sababu hadi watazamaji nao wanajiona ni wajuaji.  Pia kuna wasanii ambao wanababaisha kwenye suala zima la  uigizaji, watu wanakurupuka tu na kwenda kushuti wakati  sisi tulikuwa tunaingizwa kwenye mafunzo mpaka ujue nd’o uigize,” alisema.

Stori: Khadija Bakari

Leave a Comment