×

Lwakatare: Chadema Si Salama kwa Wapenda Maendeleo

MBUNGE wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare,  amewataka wasomi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kufanya tathmini ili kujua wanaongozwa na watu wa sampuli gani.

 

Alikuwa akihutubia  katika mkutano wa hadhara jimboni kwake ambapo  amesema, “Viongozi wa Chadema ni kama vile wana maplastiki vichwani badala ya ubongo.”

 

Amewashangaa Chadema wanavyompinga Rais Magufuli kwa mambo makubwa ya ujenzi wa miundombinu aliyoyafanikisha wakati wao ukarabati wa jengo lao la makao makuu unawashinda ilihali wanapokea mabilioni ya shilingi kama ruzuku kila mwaka.

 

Lwakatare alifukuzwa uanachama wa Chadema hivi karibuni baada ya kutotii agizo la chama hicho la kutohudhuria Bunge kutokana na #COVID19. Baada ya kufukuzwa alirejea na kujiunga na Chama Cha Wananchi (CUF).

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Leave a Comment