
MSANII wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed, Shilole amesema hajawahi ku-date na presenter wala DJ wa kituo chochote ili aweze kutusua kimuziki badala yake anajiheshimu na kuwaheshimu wanaume hiyo ndio imemsaidia kufanya nao kazi na kutusua.
Shilole amesema hayo leo Jumanne, June 9, 2020, wakati akifanya mahojiano na Kipindi cha Front Page kinachoruka kupitia +255 Global Radio.
“ROMA anapenda kutembelea trending yangu, sijawahi ku-date na DJ ili nifanikiwe kimuziki, kama yupo basi aje na vielelezo na vithibitisho, ilikuwa wapi na lini nitampa Tsh milioni 1.5.
“Ukijirahisisha wanaume wanakutumia halafu wanaambizana ‘nishapita nae huyo’, ukimheshimu mwanaume na yeye anakuheshimu, mimi nimewafanya kuwa kama brothers na mimi sisiter. Unaweza kutafuta DJ mmoja au presenter haukatazwi.
“Mwanaume lazima um-control, huwezi kumuacha tu anafanya vitu vya hovyo, zamani nilikuwa mbabe kutokana na mazingira, nilikuwa naishi kibabe kuanzia asubuhi nawaza kupigana tu, lakisni sasa hivi nimekuwa, wakati mwingine nikimzingua na yeye ndo hivyo.
“Mimi nikimfumania mume wangu Uchebe tuachana hapo hapo, sasa nisubiri nini? Na ujumbe huu anaujua.
“Wasanii wa kike wajithamini, huwezi kuonekana kila siku umevaa machupi chupi yako halafu mtu aje kuweka pesa kwako, kama unavaa chupi basi utapata brand ya chupi na hautakuwa na thamani, tuweke hadhina ya baadaye, watoto na ndugu zako watakutazamaje?
“Mimi nilichora tattoo kwa kufuata mkumbo, ulikuwa utoto tu hadi najuta. lakini kwa sababu nina safari ya Sweden nitavumilia maumivu lakini nitakwenda kuzifuta, ukiwa kijana usikurupuke, kuna nafasi nyingi mfano jeshi huwezi kwenda kama una tattoo.
“Pindua Meza maana yake fuata akili yako, using’ang’anie sehemu moja. Maisha yakiwa magumu upande mmoja badilisha fikira, fanya kitu kingine uta-make.
“Nimeshaanzisha foundation yangu ambayo nitakuwa nashughulika na akina mama na watoto, napenda wasifanye mambo ambayo yana faida ya muda mchache na madhara ya muda mrefu, wapo wanaosema kwa nini yeye alifanya acha na sisi tufanye,” amesema Shilole.