×

Championi, Spoti Xtra Watoa Ndoo, Sabuni kwa Askari Dar

MHARIRI wa Gazeti la Championi Jumatatu, Ezekiel Kitula (kulia), akimkabidhi sabuni, Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mabatini, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, ASP Juma Lujuo kwa ajili ya askari wake kunawia kwa lengo la kulinda afya zao wanapolitumikia taifa. Kushoto ni Mhariri wa Championi Ijumaa, John Joseph ambaye alimkabidhi ndoo. Wa pili kushoto ni Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally.

MAGAZETI ya michezo na burudani ya Championi na Spoti Xtra, yametoa ndoo za kunawia pamoja na sabuni kwa askari wa Kituo cha Polisi cha Mabatini, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

 

Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally, amesema vifaa hivyo ni kwa ajili ya kuwakinga askari wa kituo hicho dhidi ya Corona, wanapokuwa katika mapambano ya kulitumikia taifa letu.

 

Naye Mhariri wa Gazeti la Championi Jumatatu, Ezekiel Kitula, alisema: “Tunatambua umuhimu wa askari katika kuilinda amani ya nchi. Tunajua pasipo amani, wasomaji wetu hawawezi kusoma magazeti yetu, kwa hiyo tumetoa ndoo na sabuni hizi ili kuwawezesha askari wetu kunawa mara kwa mara ili kujikinga na virusi.”

 

Akipokea vifaa hivyo jana Ijumaa, Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mabatini, ASP Juma Lujuo, aliyashukuru magazeti ya Championi na Spoti Xtra kwa kuonyesha moyo ya kuijali jamii yao.


Huu ni mwendelezo wa magazeti ya Championi na Spoti Xtra kuonyesha kuijali jamii ya Watanzania na kuhakikisha inakuwa pamoja nayo wakati wote. Itakumbukwa kuwa magazeti haya yamekuwa yakinawisha watu mbalimbali mitaani kwa lengo la kujikinga dhidi ya Corona na kusaidia kupunguza maambukizi.

Magazeti haya pamoja na kusheheni habari motomoto zenye kuaminika, makala za kusisimua, hadithi, uchambuzi na takwimu za michezo mbalimbali, pia yamekuwa yakijitoa na kurudisha kwa jamii sehemu ya kidogo kinachopatikana.

 

Championi linapatikana mtaani kila Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumamosi kwa Sh 800 tu, wakati Spoti Xtra linapatikana kila Alhamisi na Jumapili kwa Sh 500 tu.

Na Mwandishi Wetu

PICHA: MUSA MATEJA 

 

Leave a Comment