
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Mashaka Gambo, amesema kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya Rais Dkt. John Magufuli kwa taifa hili ndani ya miaka mitano, hakuna haja ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuruhusu mtu mwingine kuwania nafasi ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Gambo amesema hayo leo Juni 13, 2020, wakati akizungumza kwenye kongamano la vijana wa CCM mkoa wa Dar es Salaam.
“Nilikwenda Karatu nikakuta mtu ananiambia ‘mimi ni CCM damudamu’, ndani kavaa fulana ya Chadema nje ya CCM, akifika sehemu kuna Chadema anavua ya CCM, akikuta kuna CCM anavaa ya CCM, huo ni unafiki. Kazi imefanywa na Rais Dkt. John Magufuli, vinaja wa CCM wanatembea kifua mbele.
“Anayoyafanya Rais Magufuli si ya kutengeneza, yanaonekana kwa macho, tangu uhuru mpaka awamu ya nne tulikuwa na hospitali wilaya za wilaya, Magufuli anajenga hispitali mpya nne za wilaya. Wakazi wa Ngorongooro, Longido, walikuwa wakienda kutibiwa Kenya, leo ni hapahapa.
“Hivi hata kama unataka demokrasia, kwa miaka hii mitano aliyofanya makubwa Rais Magufuli mpaka dunia nzima inamkubali halafu unakwenda kuchukua fomu ugombee nae, huu ni wendawazimu, demokrasia ni pamoja na kukubali kwamba huyu mtu anaweza, acha mimi nisubiri kwanza.
“Zamani tulikuwa tunapigwa virungu na mgambo siku hizi haya mambo hakuna, sijui mtu anakuja ofisini anakuuliza unanifahamu mimi…. siku hizi hakuna, kila mmoja amenyooka anafuata sheria, haya yote yameletwa na Rais Magufuli.
“Vijana wa Dar mnatakiwa mumlinde sana RC Makonda, mmepata Mkuu wa Mkoa jasiri sana kwani amejitoa mhanga hata wa maisha yake, vijana msikubali kutumika na wapinzani. Sisi wakuu wa mikoa tunamuheshimu sana RC Makonda, kwa sababu Dar ni mkoa mgumu.
“Vijana pendaneni, mshirikiane na mpeane fursa, changamoto tuliyonayo vijana wa chama chetu wanachojifunza ni unafki. Mtu akiwa mnafiki anapozeeka anakuwa mchawi… Chama Cha Mapinduzi ni chama kizuri, chenye serikali na fursa nyingi.
“Vijana wa Dar tunajisahau sana, wakati wa uchaguzi Mkuu wa 2015, majimbo mengi ya Dar, kata zilikwenda kwa upinzani. Hakuna mpinzani anayependa RC Makonda afanikiwe, na sisi vijana tunaingia kwenye huo mkumbo. Sasa tuungane waziwazi na kuwaeleza watu kwamba tunaweza.