×

Katibu Mkuu Aiagiza OSHA Kusimamia Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi

Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Bw. Andrew Massawe, akizungumza jambo wakati alipotembelea ofisi za OSHA.
Mkutano  wa Andrew Massawe na baadhi ya wafanyakazi wa OSHA ukiendelea.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda akizungumza.

 

Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) umetakiwa kuendelea kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ikiwemo kuelimisha wananchi kuhusu masuala ya Usalama na Afya kazini ili kupunguza ajali na magonjwa yanayoweza kutokea katika sehemu za kazi.

 

Agizo hilo limetolewa na Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Bw. Andrew Massawe, alipotembelea ofisi za OSHA kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa maagizo mbali mbali ya kiutendaji ambayo aliyatoa kwa viongozi wa taasisi hiyo mwezi Januari.

Aidha, Bw. Massawe ameeleza kuridhishwa kwake na utekelezaji wa maagizo yake ikiwemo kuanzishwa kwa mfumo wa kieletroniki wa usajili na usimamizi wa sehemu za kazi (WIMS), programu mbali mbali za kuelimisha wananchi pamoja na kuboresha tovuti.

Awali, Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, alitoa mrejesho wa utekelezaji wa maagizo ya Katibu Mkuu katika taarifa yake aliyoiwasilisha katika kikao baina ya menejimenti ya OSHA na Katibu Mkuu huyo.

OSHA ni taasisi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana,Ajira na wenye Ulemavu ambayo ina jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2003 ambayo inalenga kuboresha mazingira ya kazi hapa nchini.

Leave a Comment