
ASILIMIA 96 ya vifaa tiba na dawa vinatoka nje, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kuwa uhaba wa dawa sababu ya ugumu wa kusafirisha kuja nchini kutokana na Corona. Lakini Serikali imejitahidi kwa sasa kuna viwanda vya dawa kama 4 nchini.
Hayo yamesemwa leo Jumatatu, Juni 15, 2020, na Rais wa Chama cha Wafamasia, Issa Hango wakati akifanya mahojiano na Kipindi cha Front Page kinachoruka kupitia Global Radio.
“Kuna dawa muhimu ambazo hutakiwi kuzikosa kama Taifa. Huwezi kuwa na zote lakini kama inawezekana ni lazima ziwepo na zizalishwe hapa nchini.
“Bado tunahitaji kuendelea kuongeza watalam na sio tu kuongeza watalam, watalam bora. Ndio maana kuna baadhi ya vyuo vilifutiwa usajili.
Taaluma ya dawa za asili zinahitaji uwekezaji mkubwa, Serikali iwekeze au watu binafsi. Changamoto inayotusumbua sisi ni raw material ya kutosha.
Dawa za ARV kuziiba na kupekea kwenye mifugo ili inenepe haraka ni jambo baya sana, watu hawa hawajui maadili ya Ufamasia. Kulikuwa na wizi wa dawa, wahusika walimaktwa na kufutiwa usajili, si wafamaisa tena,” Rais wa Chama cha Wafamasia, Issa Hango.