
HATIMAYE mshambu liaji wa Yanga, David Molinga, amemuomba radhi kocha msaidizi wa timu hiyo, Charles Boniface Mkwasa na sasa mambo yamekuwa freshi.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuibuka kwa taarifa kwamba wawili hao hawaelewani hali iliyosababisha Molinga asisafiri na wenzake kwa basi kwenda Shinyanga kucheza dhidi ya Mwadui na badala yake akaondoka na Kocha Mkuu, Luc Eymael kwa ndege.
Kitendo cha Molinga kukataa kusafiri na wenzake, kiliwaudhi wengi, ndiyo maana juzi kukawa na kikao kizito ambacho mwisho wa siku mshambuliaji huyo raia wa DR Congo kuomba msamaha na mambo kuisha.
Mbali na Mkwasa, Molinga pia aliwaomba radhi wachezaji wenzake pamoja na uongozi kutokana na tukio hilo ambalo lilianza kuwagawa.
Akizungu mza na Spoti Xtra, meneja wa timu hiyo, Abeid Mziba, alisema: “Viongozi tulikaa na kuzungumza na wachezaji ili kuwekana sawa, kwa sababu lengo letu ni kuijenga timu iweze kufanya vizuri.
“Kizuri ni kuwa Molinga amekiri kuwa alikosea na ameomba msamaha ambapo hivi sasa kila kitu kipo sawa.”
Juzi wakati Yanga ikicheza mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Molinga alianzia benchi.
ISSA LIPONDA, DAR