
Balozi Ali Karume amekuwa wa pili kujitokeza kuchukuwa fomu ya kuwania kugombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Aidha, Mbwana Bakari Juma amekuwa mwanachama wa kwanza wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuchukua fomu ya kugombea urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mwaka huu. Rais Dkt. Ali Mohammed Shein ataondoka madarakani baada ya kuongoza kwa vipindi viwili (miaka 10) kwa mujibu wa katiba.