×

Yanga yatua Bungenio Bila Morrison

WACHEZAJI na viongozi wa Yanga leo Juni 15, 2020 wamefika Bungeni Dodoma wakitokea Shinyanga baada ya mchezo wa Ligi kuu dhidi ya Mwadui FC uliopigwa Jumamosi na Yanga kushinda goli 1-0.

 

Spika Job Ndugai amewakaribisha na kuwatambulisha na wabunge wakawashangilia huku wakimulizia Bernard Morrison ambaye hajaambatana na timu.

 

Spika amewapongeza Yanga wa ushindi dhidi ya Simba Machi 8, 2020 ambapo pia akawaomba wabunge wa Simba wawapigie makofi wachezaji na viongozi wa Yanga waliofika Bungeni hapo.

Leave a Comment