×

Eymael Afunguka Ishu ya Morrison Kutua Simba

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mbelgiji, Luc Eymael, ameamua kuvunja ukimya na kuweka wazi juu ya hatma ya winga wa kikosi hicho, Mghana, Bernard Morrison, ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na Simba.

 

Ikumbukwe kuwa, tangu Machi, mwaka huu kulikuwa na taarifa zilizokuwa zikimhusisha Morrison kujiunga na Simba, wiki iliyopita kupitia mitandao ya kijamii, Morrison alisikika akidai kuwa alipewa dola 5000 (milioni 11, 560, 000), ikiwa kama sehemu ya kumshawishi atue Simba.

 

Eymael aliliambia Championi Jumatano,kuwa, Morrison hawezi kwenda Simba kwa sababu tayari ameshasaini Yanga na kama ikitokea akasaini Simba basi atafungiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), kwa muda wa miaka miwili.

 

“Unajua Morrison tayari ameshasaini Yanga, hawezi tena kwenda Simba, kama ikitokea akasaini Simba, basi ni lazima atafungiwa na FIFA, kwa muda wa miaka miwili kama ambavyo sheria inasema,” alisema Eymael.

 

Mpaka sasa Morrison hajajiunga na kikosi cha Yanga kilichopo mkoani Dodoma kikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa leo katika Uwanja wa Jamhuri.

Stori: Abdulghafal Ally, Dar es Salaam

ERASTO NYONI “NIMECHOKA Nitawajibu Nikiwa Uwanjani /Nafuata Maelekezo ya Kocha”

Leave a Comment