×

Samatta Kumvaa Kipa Wa Man United Leo Usiku

STRAIKA wa Aston Villa, Mtanzania Mbwana Samatta leo Jumatano ataanza kazi ya kuipambania timu hiyo kutoshuka daraja kwa kupambana na Sheffi eld United inayochezewa na kipa Dean Henderson aliye kwa mkopo akitokea Manchester United.

 

Samatta atakuwa na kibarua hicho kwenye mechi ya Ligi Kuu ya England ‘Premier’ ya kwanza baada ya ligi hiyo kuruhusiwa kuendelea kutokana na kusimama kwa miezi mitatu kutokana na uwepo wa Virusi vya Corona.

Mtanzania huyo ambaye ana bao moja katika Premier, tangu ajiunge na Aston Villa katika dirisha dogo ataiongoza timu yake kusaka pointi tatu wakiwa nyumbani Uwanja wa Villa Park.

 

Mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu na Watanzania wengi kwa kumuona staa wao huyo ambaye ni nahodha wa timu ya taifa, Taifa Stars, ataendelea na moto gani baada ya ligi hiyo kusimama kwa miezi miwili.

 

Aston Villa inapambana kutoshuka daraja ambapo kwa sasa ipo nafasi ya 19 ikiwa na pointi 25 wakati Sheffi eld United ikiwa nafasi ya saba na pointi 43.

Stori: Said Ally, Dar es Salaam

Leave a Comment