Rais Dkt. John Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amechukua fomu ya kuwania kinyang’anyiro cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Magufuli amekabidhiwa fomu hiyo na katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally, Makao Makuu ya CCM, Dodoma.