×

Grace Matata Aachia Dude ‘Me and You’ (New Lyric Video)

MSANII wa muziki kutoka Tanzania, Grace Matata jana Jumatano 17 Juni 2020 alitangaza kuachia kazi mpya na ya kwanza kwa mwaka huu wa 2020 ikiwa ni wimbo wa kwanza kabisa kusikika kutoka kwenye EP project ya REBIRTH.

 

Wimbo huo ambao umetoka jana unakwenda kwa jina la ‘Me and You’ na ni miongoni mwa nyimbo nne (4) zinazopatikana kwenye EP project ya REBIRTH. Kazi hiyo mpya imefanyika kwenye studio za Fisher Records zilizopo Kunduchi, Dar Es Salaam chini ya Mtayarishaji wa muziki Taz Goemi.

 

Akiongelea juu ya wimbo huo, Mtayarishaji huyo wa muziki anasema: “Me and You ni wimbo fulani wa kuchangamka kidogo, mahadhi yake yamekaa ki-afrobeat na pop. Ukisililiza utasikia miondoko ya Pop, jazz na fusion ya Afro-beats.

 

Grace alitamani awe na wimbo wa aina hii kwenye project yake mpya, wimbo fulani umechangamka lakini pia uwe soft kwenye masikio, wimbo ambao ukiwa sehemu na marafiki unaweza enjoy lakini ukiwa peke yako nyumbani pia utaweza uenjoy. It’s an exciting vibey song.” – Taz Goemi (Fisher Records/ Music Producer).

 

Akizungumzia pia juu ya wimbo huo, Grace anasema: “Baada ya kurekodi nyimbo kadhaa nilikaa na Taz na kumwambia tunahitaji wimbo wa kuchangamka kidogo, wimbo ambao mtu akinisikia awe suprised kidogo na kile nilichokifanya but aenjoy at the same time, maana watu wengi wanajua nyimbo zangu ni za taratibu sana, and idea ya hii EP inayotarajia kutoka is to show upande tofauti wa Grace Matata.

 

So nilimwambia natamani kifanya kitu cha kuchangamka, kitu ambacho mtu awe sehemu ya starehe na marafiki aweze kufurahia kucheza na akiwa home aweze kuenjoy wimbo pia.

 

He played me several beats nikawa sipati feeling nayoitafuta au nayoitaka, tukaamua kutengeneza beat mpya from scratch, idea moja ikazalisha nyingine and the beat slowly came together nicely, baada ya siku kadhaa nikapata idea ya nini nachotaka kuimba kwenye hiyo beat nikapanga session, nikarudi studio na kuingiza vocals.

 

I had a lot of fun making Me and You, it’s short and sweet na ni miongoni mwa nyimbo kwenye EP yangu ambazo nazicheza mara kwa mara”. – Grace Matata.

 

Akigusia pia juu ya wimbo huo, Meneja wa Muziki Tanzania, Ms Brown amesema: “I Love this song simply because it’s fresh and catchy. Nimependa Taz alichokifanya na jinsi alivyomchangamsha Grace kwenye huu wimbo.

 

Kusema ukweli nilikuwa a bit worried mwanzoni kama kweli tungeweza kumuweka Grace kwenye wimbo ambao unakimbia kidogo, ila yeye alikuwa ana nia ya kufanya hichi kitu na kwa upande wangu nia haikuwa hasa kufanya ngoma ya kuchangamka kiivyo bali kutengeneza wimbo utakao-balance mazingira yote.

 

Shabiki akiwa out with friends, in a party, a club or hata home aweze piga wimbo na kuenjoy. I believe music can serve a 360 purpose and maintain longevity.

 

Hicho ndicho nilichokuwa nakitafuta mimi hasa sio tu kwa huu wimbo bali nyimbo zote za kwenye hii Project. Kwa upande wetu naamini tumefanikisha hilo sasa ni Watanzania kutupa kura yao”. – Ms Brown (Artist Manager / Grace Matata).

 

Me and You’ single ya kwanza ya Grace Matata kutoka kwenye EP ya REBIRTH kwa sasa inapatikana kwenye digital platforms zote kuanzia mchana wa jana, vile vile official Lyric video ya wimbo huo upo kwenye YouTube channel ya Grace Matata.

 

Leave a Comment