
Rais wa HONDURAS, Juan Orlando Hernández ambaye pia anaugua #COVID19, amelazwa akipatiwa tiba ya Homa ya Mapafu (Pneumonia).
Rais Hernández (51) amelazwa Hospitali ya Jeshi na anapatiwa dawa kwa kutumia dripu. Msemaji wa Taasisi ya Afya ya SINAGER, Francis Contrares amesema hali ya Rais huyo ni nzuri.
Rais Hernández alitangaza kuwa yeye, Mkewe Ana García Carías na wafanyakazi wake wawili wameambukizwa.