×

LaCreamena Msanii wa Congo Kuliteka Soko la Afrika

LaCreamena (Gracia) ni mwanamuziki  wa Jamhuri ya Kidemorasia ya Congo anayefanya kazi zake nchini Australia na ambaye anatamba na kibao chake  kiitwacho OIOIOI ambacho kiliipuliwa Mei 22, 2020, akiwa amepania kuliteka soko la muziki la Afrika.

Mbali na muziki, LaCreamena anapenda kutembea sehemu mbalimbali  na kukutana na marafiki na watu wa familia mbalimbali.

“Kilichonisukuma kufanya muziki ni upendo, harakati na njia ya kuiweka jamii katika mazingira ya uhuru,” anasema mwanamuziki huyo ambaye singo yake hiyo iko katika lugha ya Kilingala.

 

“Muziki hunifanya nijihisi nina nguvu kubwa katika kufanya mambo mema, hunifanya  niwajaze mashabiki wangu nguvu za  kujiamini,” alisema msanii huyo ambaye singo yake hiyo inapatikana katika video iliyo hapo chini.

Leave a Comment