×

Aika Navykenzo Aomba Msaada Aolewe

MWANAMUZIKI memba wa Kundi la Navykenzo, Aika Mariale amesema kuwa kwa hivi sasa wanahitaji msaada wa ushauri wa watu mbalimbali kuhusu wao kufunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi Nahreel, maana ndiyo kitu muhimu.

 

Akipiga stori na Risasi Jumamosi, Aika alisema kuwa wamekaa zaidi ya miaka kumi na mzazi mwenziye Nahreel bila kusikia kelele za watu wakisema wafunge ndoa, basi wanaweza kupiga miaka mingine kumi, hivyo ushauri wa watu ni tiba kubwa kwao.

“Yaani sasa hivi kinachotakiwa kabisa kwetu ni ushauri wa kila siku, hiyo ndiyo tiba kwa kweli maana unaweza tu ukapenya siku moja na hapohapo tukaamua kwenda kanisani maana pia ndoa ni watu wawili na anayetufungisha,” alisema Aika ambaye tayari ana watoto wawili na Nahreel; Gold na Jamaica.

STORI NA IMELDA MTEMA

KIJANA ATOA USHUHUDA MZITO “NILIMSHIKIA PANGA MAMA YANGU/WALINIVISHA TAIRI WANICHOME MOTO”

Leave a Comment