×

Congo: Msaidizi Wa Rais Jela Miaka 20 Kwa Ufisadi

Kwa mara ya kwanza Kongo inashuhudia vigogo wakipewa adhabu zinazowastahili kwa makosa waliofanya, na Vital Kamerhe ambaye ni msaidizi mkuu wa Rais amekuwa mfano wa kwanza kwa kushtakiwa na kuhukumiwa kwa ufisadi.

Msaidizi mkuu huyo wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela na kazi ngumu kutokana na kukutwa na hatia ya ufisadi.

Vital Kamerhe, mwenye umri wa miaka 61 alitiwa hatiani kwa ufisadi wa zaidi ya dola milioni 50 kwa mujibu wa mahakama kuu ya mjini Kinshasa.

Fedha hizo zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya kujenga nyumba 1,500 ambapo ilikuwa ni mpango Rais Tshisekedi aliyetangaza programu hiyo Januari 2019 mara baada tu ya kuapishwa kuwa Rais.

Leave a Comment