×

Mwanamitandao aliyekuwa milionea akiwa na miaka 15 afariki

MWANAMITANDAO chipukizi nchini Russia, Anastasia Tropitsel (18) aliyeupata umilionea akiwa na umri wa miaka 15, amekufa katika ajali ya pikipiki, huko Bali, Indonesia.

Tropistel ambaye jina lake halisi ni Anastasia Zubrina, amefariki kutokana na majeraha ya kichwa wakati pikipiki yake aina ya Kawasaki Ninja 250 ilipoanguka kwa kugonga fensi iliyokuwa kando ya barabara baada ya kushindwa kuidhibiti pikipiki hiyo akiwa katika spidi ya maili 60 kwa saa.

Hayo yalisemwa na rafiki yake wa kiume Viktor Maydanovich (30) ambaye naye alikuwa anaendesha pikipiki nyingine.

Anastazia alianza kuendesha blog tangu akiwa na umri wa miaka 12 na akaelezea alivyokuja kuwa milionea katika umri wa miaka 15 hasa kwa kutumia intaneti.

Kaulimbiu yake kuu kwa wafuasi wake katika mitandao ilikuwa ni: “Nawatia moyo mfanye mambo ambayo mnafikiri hamwezi kuyafanya.”

Tropistel alikuwa Bali wakati wa  kipindi cha ‘lockdown’ ili kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 ambapo alikuwa amekwenda kutafuta habari mbalimbali kwa ajili ya Instagram yake.

 

Blog ya Tropistel iliwataka wafuasi wake  kujikita na kuyafanya mambo ambayo huwaletea hisia za woga ili kujipa uwezo wa kutoogopa kufanya chochote.

 

Leave a Comment