
BAADA ya Roy Keane kum-shambulia kipa David de Gea kwa kuwa na makosa mengi yanayoigharimu Manchester United, kipa wa zamani wa Premier, Mark Schwarzer, naye amesisitiza kuwa Mhispania huyo anafi kirisha.
De Gea aliruhusu shuti la winga Steven Bergwijn kuchomoka mikononi mwake na kuruhusu bao kwa Tottenham dhidi ya United juzi Ijumaa, kabla ya Bruno Fernandes kusawazisha kwa penalti na kufanya matokeo ya 1-1.Schwarzer, amesisi-tiza kuwa sasa De Gea atakuwa kwenye presha kubwa ya kupata namba kwenye timu hiyo pindi Dean Henderson ataka-porejea akitokea kwa mkopo Sheffi eld United.

“Kwa zaidi ya miezi 18 iliyopita, De Gea ameshafanya makosa mengi sana na hilo halitara-jiwi kwa kipa wa levo kama yake,” alisema Schwarzer, ambaye ali-zichezea Middlesbrough, Fulham, Chelsea na Leicester kwenye Pre-mier. “Kwa kipa wa kiwango cha dunia, makosa yanayosababisha bao yanatakiwa yasizidi mawili msimu mzima na kwa hakika ameshafanya makosa mengi zaidi ya hayo.
“Hali itambadilikia wakati Dean Henderson atakaporejea na anacheza vizuri sana huko Sheffi eld United na ameshaweka wazi kuwa hatakaa benchi.” Lakini Keane alikwen-da mbali zaidi aliposema juu ya De Gea: “Nime-choshwa hadi kufi kia kiwango cha mwisho juu ya kipa huyu.
Ningekuwa mimi ningekuwa nago-mbana naye kila mara mapumziko, ningem-chapa ngumi kadhaa. Huyu ni kipa wa kimatai-fa, unatakiwa kuonyesha hadhi yako uwanjani.”