×

Azam yazindua Tamthilia Nne Kurushwa Chanel ya Sinema Zetu

Mkali wa filamu za kiasili, Madebe Lidai akisisitiza jambo baada ya kupata nafasi ya kuzungumza kwenye hafla hiyo.

AZAM Media kupitia kwa mkurugenzi wake, Tido Mhando, jana walizindua tamthilia nne ambazo zitarushwa kwenye Chanel 103 ya Sinema Zetu ukiwa ni mpango endelevu wa kuleta ushindani kwenye masuala ya fi lamu kitaifa na kimataifa.

Msanii Vicent Kigosi ‘Ray’ akizungumza wageni waalikwa waliokuwa wakimsikiliza.

Uzinduzi huo ulifanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar na kuhudhuriwa na waigizaji wakongwe na chipukizi ambao wamehusika kwenye tamthilia hizo.Akizungumza katika uzinduzi huo, Mhando alisema:

 

“Tunarejea upya na tulianza mpango huu tangu mwishoni mwa mwaka 2019, na sasa kazi imeanza, malengo makubwa ya Azam TV ni kuona tunaweza kushindana na wenzetu walioanza ikiwa ni wale wa Ghana na Nigeria.

Baadhi ya wasanii wakiwa kwenye picha ya pamoja.

”Mhando alizitaja tamthilia hizo kuwa ni Panguso na Single Mama ambazo zitarushwa kuanzia Julai 13, mwaka huu kila siku za Jumatatu hadi Alhamisi.

 

Nyingine ni Shilingi itakayorushwa Ijumaa na Jumapili saa 3 usiku kuanzia Julai 17 sambamba na Tandi.

 

Muigizaji Vincent Kigosi maarufu Ray ambaye ni miongoni mwa waigizaji waliozungumza katika uzinduzi huo, alisema walikuwa kimya kwa muda mrefu kutokana na kukosa ushindani, hivyo Azam TV kupitia Chaneli ya Sinema Zetu watarejesha makali yao.

PICHA NA RICHARD BUKOS

Leave a Comment