
WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe, amesikitishwa na kitendo cha mashabiki walioingia Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, jana kushuhudia mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Mbeya City na Simba kutochukua tahadhari dhidi ya corona.
Mwakyembe ambaye alifika uwanjani hapo na kushuhudia mchezo huo, alisema:

“Kwa nje usimamizi upo vizuri maana kuna maji na sabuni watu wanawa, pia mashabiki wanavaa barakoa, lakini ndani watu hawajali, wanaona kama corona imeisha.

Lazima tutachukua hatua kama tulivyofanya huko nyuma,”Ikumbukwe kuwa, hivi karibuni Serikali ilitangaza kuwazuia mashabiki kuingia kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma baada ya kujazana na kutochukua tahadhari wakati wa mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya JKT Tanzania dhidi ya Yanga iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1
STORI: JOHN JOSEPH – SPOTI XTRA