
TIMU ya masoko ya Global Publishers wachapishaji wa Magazeti ya michezo ya Championi na Spoti Xtra ambayo ni namba moja kwa mauzo pamoja na Habari za uhakika leo Juni 27, 2020 waliwatembelea wateja wake maeneo ya Mabibo Sokoni kuwahamasisha kuendelea kushiriki kwenye Promosheni ya Shinda gari ambayo ndo habari ya mjini.
Ofisa Mkuu wa kitendo cha Masoko, Anthony Adam amewaambia wasomaji hao ambao walikuwa wakigombania nakala za magazeti kwa wingi kuwa waendelee kujaza kuponi kwa wingi kwa kuwa mshindi wa gari anatarajiwa kutangazwa rasmi Julai Mosi.

Kabla ya mshindi wa gari kutangazwa kuna washindi wengine ambao walijivunia mkwanja wa kutosha pamoja na simu ikiwa ni lengo la kurejesha shukran kwa wanunuzi wa magazeti ya Championi na Spoti Xtra.
“Kila kitu kinakwenda sawa na tayari maandalizi ya kutoa zawadi kubwa ambayo ni gari yameshakamilika, kinachotakiwa kufanyika ni wateja kuendelea kununua magazeti ya Championi na Spoti Xtra ambapo kuna kuponi Ukurasa wa pili inahitaji kujazwa.

“Mteja akishajaza taarifa zake Kwenye nakala halisi ya Gazeti na sio kivuli anakuwa ameshiriki tayari shindano anapaswa ampe kuponi wakala aliye karibu naye ama anaweza kuleta kuponi makao makuu ya Global Group, Sinza Mori hata kutuma kwa njia ya Posta na kuponi zote zilizochezwa Kwenye droo zilizopita zitatumika Kwenye droo kubwa ya mwisho ambayo itamtoa mshindi wa Shinda Gari,” alisema.

