×

Makonda,Atoa Mwezi Mmoja,Mkandarasi kumaliza ujenzi Wa jengo la Manispaa ya Ubungo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amegoma kukabidhi kwa Chama cha Mapinduzi CCM Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Manispaa ya Ubungo kutokana na ujenzi huo kusuasua hadi sasa ambapo amemtaka Mkandarasi wa ujenzi huo Wakala wa Ujenzi TBA kuhakikisha anakabidhi mradi ndani ya mwezi mmoja kuanzia Leo.

RC Makonda ameyasema hayo baada ya   kuona ujenzi huo ambao ulitakiwa kukamilika na kukabidhiwa Mwezi Disemba mwaka jana lakini mkandarasi aliomba kuongezewa miezi sita lakini hadi sasa Ujenzi haujakamilika jambo lonaloendelea kuwafanya Watumishi wa Manispaa hiyo kufanya kazi katika mazingira magumu.

Akizungumza na Global Publishers Makonda amesema kuwa atachua hatua endapo mkandarasi hatomaliza baada ya huo mwezi mmoja.

“Kwa sasa tunaendelea kukabidhi miradi  kwa Chama Cha Mapinduzi CCM ambapo kwa siku ya leo amekabidhi miradi yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 196.4 kwa upande wa Jimbo la Kibamba.

“Leo nakabidhi Mradi Wa Standi ya Mabasi ya Mikoani ambayo ipo Mbezi Luis na imegharimu Bilioni 50, Upanuzi wa Barabara ya Kimara hadi Kibaha yenye urefu wa Km 19.2 na gharama ya Bilioni 140.4, Upanuzi wa Mtambo wa Maji Ruvu Juu na ujenzi wa Tank Kibamba wa thamani ya Milioni 624.

Kwa hiyo nawasihi muulinde hii miradi yote kwa sababu inatusaidia wote haichugui ikiwa ni Wafanyabiashara wadogo,wakina mama tunawashusha ndoo kichwani na pia Afya ya mama na mtoto,”alisema Rc Makonda.

Aidha RC Makonda pia amekabidhi mradi wa Ujenzi wa Mabanda Saba ya Wafanyabiashara Mbezi Luis unaogharimu Bilioni 1.5 na Ujenzi wa Kituo cha Afya Kimara Bilioni 1.5.

Leave a Comment