×

Cioaba: Kufungwa Tena Na Simba Itakuwa Aibu

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba, amesema kuwa litakuwa jambo baya sana kwao na aibu kama watashindwa kupata ushindi mbele ya Simba kwenye mchezo wa robo fainali utakaopigwa leo Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

 

Cioaba amesema walipoteza kwenye michezo yote ya ligi kuu waliyocheza na Simba msimu huu, lakini mbali na hivyo wamekosa ushindi kwenye michezo mitatu ya ligi kuu waliyocheza hivi karibuni, hivyo ili kurejesha morali kwenye timu yao wanatakiwa kushinda kwenye mchezo huo na kusonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali.

Akizungumza na Championi Jumatano, Cioaba amesema mchezo huu ni muhimu sana kwao kushinda kwa sababu wanahitaji kuwa mabingwa wa Kombe la FA, lakini mbali na hivyo itakuwa ni jambo baya kwenye timu hiyo kama watashindwa kupata ushindi tena kama ilivyotokea katika michezo miwili ya ligi kuu na kuongeza kuwa kupata ushindi kwenye mchezo huo kutawaongezea morali wachezaji wake.

 

“Tunahitaji kupata ushindi kwenye mchezo huu, kwa sababu nia na malengo yetu ni kushinda Kombe la Shirikisho, hatuwezi kulipata kama tutafungwa tena na Simba, itakuwa aibu sana kwetu.

 

Mbali na hivyo hatujashida katika michezo mitatu ya ligi kuu iliyopita, hivyo tunahitaji ushindi kwa hakika katika mchezo huu,” alisema Cioaba.

 

Azam wamekosa ushindi kwenye michezo mitatu ya ligi kuu, walitoka suluhu na Yanga, kisha wakafungwa bao 1-0 na Kagera ugenini, kisha wakapata sare ya bao 1-1 na Biashara United.

Leave a Comment