
Mpinzani wa Rais Donald Trump, Joe Biden amesema hatoendesha kampeni za Urais wakati huu ambapo nchi hiyo inakabiliana na janga la #COVID19
Biden aliyekuwa Makamu wa Rais katika kipindi cha utawala wa Rais Barack Obama, amesema atafuata maelekezo ya wataalamu sio kwa ajili yake tu bali kwa nchi nzima.
Mwishoni mwa mwezi Juni, Rais Trump alifanya kampeni huko Tulsa jijini Oklahoma ambapo tofauti na matarajio, watu wachache walijitokeza na alishindwa kujaza ukumbi wa watu 19,000.
Wakati huo huo, Mtafiti Mkuu wa magonjwa Dkt Anthony Fauci ameliambia Bunge la Seneti kuwa hatashangazwa endapo maambukizi mapya 100,000 yakirekodiwa kwa siku moja.
Dkt. Fauci amesema bado hawajafanikiwa kudhibiti ugonjwa huo na Wamarekani kuvaa barakoa na kuepuka mikusanyiko pekee haitoshi. Hadi sasa Marekani imerekodi visa 2,868,012 na vifo 132,834 huku waliopona wakiwa 1,084,341