
BENKI ya Dunia imeitangaza rasmi Tanzania kuingia kwenye orodha ya nchi zenye uchumi wa kipato cha kati.
Tanzania inaingia kwenye orodha hiyo ikiwa ni miaka mitano kabla ya lengo la dira ya taifa ya maendeleo ya mwaka 2025.
”Benki ya Dunia leo tarehe 01 Julai, 2020 imeitangaza Tanzania kuingia UCHUMI WA KATI. Nawapongeza Watanzania wenzangu kwa mafanikio haya.Huu ni ushindi mkubwa na kazi kubwa tumeifanya, tulipanga kuingia uchumi wa kati ifikapo 2025 lakini tumefanikiwa 2020. MUNGU IBARIKI TANZANIA” – amesema Rais Magufuli kupitia ukurasa wake wa Instagram.



The World Bank is to officially declare Tanzania a middle income country as of 1st July 2020. Jumuiya ya Afrika Mashariki sasa inakuwa na mataifa mawili kwenye kundi la MICs.
Swali: Itakuwaje kuhusu East African Community – European Union Economic Partnership Agreement? Maana Tanzania iligoma ikiamini kwamba italindwa na ile special arrangement kwa nchi maskini. Yetu macho!
Hongereni watanzania!