×

Irene Robert: Sijaolewa Bado Jamani!

Licha ya urembo alionao, Mwanamuziki wa Nyimbo za Injili nchini, Irene Robert, amesema bado hajaolewa kama watu wengi wanavyomzushia ila yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na Mungu akipenda atafunga ndoa na mpenzi wake huyo.

Irene ambaye anatamba hivi sasa na ngoma yake mpya ya Nivushe, amesema wakati wa Mungu ndio wakati sahihi zaidi hivyo ukifika basi atauaga ukapela.

Kuhusu historia yake ya muziki, Irene amesema amezaliwa na kukulia kwenye familia ya wacha Mungu, na alianza kuimba kwaya kanisani tangu akiwa mdogo na ndoto yake kubwa ilikuwa ni kuwa mwanamuziki mkubwa kama ilivyo sasa.

Leave a Comment