×

Wamarekani Wazidi Kuchukizwa, Waliangusha Sanamu la Columbus

KUNDI la waandamanaji nchini Marekani limeangusha sanamu la Christopher Columbus na kulitupa majini kwenye bandari ya mjini Baltimore jana usiku, baada ya Rais Donald Trump kuahidi kulinda mwenendo wa maisha ya Wamarekani ulioanzishwa kufuatia Columbus kuligundua bara la Amerika.

 

Wimbi la maandamano lilianza nchini Marekani, baada ya polisi kumuua Mmarekani mweusi George Floyd Mei 25.

 

Waandamanaji wamekuwa wakitaka kuondolewa kwa masanamu mengi ya kihistoria yenye utata, ikiwa ni pamoja na sanamu la Columbus na ya watu wengineo ambao wanasema walihusika na ukandamizaji kwa karne kadhaa.

 

Columbus anayesifiwa kwa kuligundua bara la Amerika, hivi karibuni wanahistoria na wanaharakati wanasema alihusika pia katika utumwa, unyonyaji na ukandamizaji  na umwagaji damu wa watu asili.

 

Leave a Comment