
Unapozungumzia watu wanaofaidi mema ya nchi, kamwe huwezi kuacha kumtaja bilionea wa Nigeria, Ismaila Mustapha ‘Mompha’ ambaye ni mtu wa karibu wa staa wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto ‘Misa’, Gazeti la IJUMAA linakuletea habari kamili.
UTAJIRI WAKE GUMZO
Jamaa huyo ambaye Wabongo wengi walikuwa hawamjui, anatajwa kuwa na ukwasi wa kutosha; ana utajiri usiopungua Dola za Kimarekani milioni 15 (zaidi ya shilingi bilioni 34.7 za Kitanzania).

MAGARI YA KIFAHARIU
maarufu wa tajiri huyo unachagizwa zaidi na aina ya magari ya kifahari anayoyamiliki ambapo inaelezwa kuwa anamiliki; Rolls-Royce, Bentley, Mclaren, Ferrari na Lamborghini.Lakini kama hiyo haitoshi, hivi karibuni anatajwa kununua mkoko mpya unaokwenda kwa jina la Rolls Royce Wraith Eagle VIII (toleo la mwaka 2020).
ANAMILIKI DUKA LA KUBADILI FEDHA
Kigogo huyo anayetajwa kuwa ni baba wa watoto wawili, mitandao mbalimbali ya Nigeria ikimuonesha na miliki duka kubwa la kubadilishia fedha la Mompha Bureau De Change lililopo Lagos-Island nchini Nigeria.
Tajiri huyo anatajwa pia kumiliki maduka madogo ya kubadilishia fedha, lakini pia anamiliki mijengo kadhaa ya kifahari nchini Nigeria.

MAONI KAMA YOTE
Maoni mbalimbali ambayo yametupiwa kwenye habari zinazomhusu, yamekuwa yakimjadili zaidi juu ya kufuru zake za magari ya kifahari anazozionesha kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram.
Wengi wamekuwa wakihoji kuhusu jeuri hiyo ya fedha kulinganisha na vyanzo vyake vya mapato wakidai kama haviendani.
UHUSIANO WAKE NA MOBETO
Uhusiano wa Mobeto na Mompha, umeanza muda mrefu ambapo vyanzo mbalimbali vinaonesha kwa mara ya kwanza walikutana Nigeria na kuponda raha pamoja mwaka jana.
Kuna vipande vya video ambavyo viliwahi kusambaa vikimuonesha mrembo huyo akiyarudi magoma akiwa na kigogo huyo kwenye moja ya kumbi starehe.