×

Serikali Kuanza Kutoa Tuzo kwa Wasanii

SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeanza mchakato wa kuandaa tuzo kwa wasanii ambazo zitajumuisha sekta zote ndani ya wizara hiyo ikiwemo habari, utamaduni, sanaa na michezo.

 

Akizungumza na shirika la utangazaji la TBC katika kipindi cha Serebuka, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa, Dkt. Emmanuel Ishengoma, amesema wamesikia kilio cha wasanii akiwemo msanii Harmonize ambaye ametoa ombi lake kwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kuendeleza utaratibu wa kutoa tuzo kwa wasanii ili kuongeza ushindani ulio wa kweli na kuhamasisha wasanii kufanya kazi zenye weledi na ubora zaidi.

Chanzo: TBC

Leave a Comment