×

Tanzia: Mwanasiasa Mkongwe, Balozi Lusinde Afariki Dunia

MWANASIASA mkongwe, Balozi Job Lusinde (90) ambaye alikuwa mmoja wa baraza la kwanza la mawaziri la Mwalimu Julius Nyerere baada ya uhuru, amefariki dunia alfajiri ya leo Jumanne, Julai 7, 2020, katika Hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.

 

Familia ya Lusinde na Malecela imesema taratibu za mazishi zinaendelea katika makazi yake, Kilimani, jijini Dodoma. Lusinde ni kaka wa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, John Malecela.

 

Lusinde aliyezaliwa Oktoba 9, 1930, aliwahi kuwa Waziri wa Mawasiliano mwaka 1965 na ni miongoni mwa watu waliofanya kazi kwa ukaribu na Mwalimu Julius Nyerere kama Waziri wa Serikali za Mitaa mwaka 1961. Pia, aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini China kuanzia mwaka 1975 hadi mwaka 1984.

 

Mawaziri wa Tanganyika mwaka 1961 baada ya uhuru;

Oscar S.Kambona (35) – Waziri wa Mambo ya nje na Ulinzi

Job M.Lusinde (32) – Waziri wa Mambo ya Ndani

Amir H.Jamal (41) – Waziri wa Mawasiliano

Paul Bomani (38) – Waziri wa Fedha

Alhaj Tewa Said Tewa (37) – Waziri wa Ardhi

Nsilo Swai (35) – Waziri wa Viwanda

Bhoke Munanka (34) – Waziri Ofisi ya Rais, Usalama wa Taifa

 

Leave a Comment