×

Tigo na Tecno wazindua Tecno Spark 5 saba saba

Meneja Bidhaa za Intaneti-Tigo Mkumbo Myonga akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa simu Mpya ya TecnoSpark5

Kampuni ya mawasiliano ya tigo imewataka wananchi kutumia nafasi ya uwepo wa maonesho ya kibiashara ya 44 ya Dare salaamu sabasaba kwa ajili ya kufanya manunuzi ya vifaa vya mawasiliano vyenye ubora kufuatia maonesho hayo kuhusisha kampuni za mawasilianobza simu ambazoZinaleta vifaa vyenye ubora

 

Meneja mawasiliano kutoka kampuni ya Tecno Erick Mkomoye akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa  zinduzi wa simu Mpya ya TecnoSpark5 ambapo  Mteja atanunua kwa bei ya laki 333,000 na kupata  ofa za kifurushi cha GB 78  kwa mwaka mzima.

Akizungumza leo jijini Dare salaamu Meneja wa bidhaa za intaneti kutoka tigo mkumba myonga  amesema katika maonesho hayo wameingia makubaliano na baadhi ya kampuni za uuzaji vifaa vya simu ambazo zina sifa na ubora kwa matumizi ya watanzania.

Kwa upande wake Meneja mawasiliano kutoka kampuni ya Tecno Erick mkomoye ameeleza kuwa hivi Sasa Watanzania wanahitaji teknolojia za Hali ya juu kwenye simu zao  wanazotumia ili kuendeleza uchumi wa Kati uliofikiwa na kuifanya endelevu  na kwa kutambua hilo wameamua kuja na simu aina ya Tecno spark 5 yenye thamani sawa na mahitaji ya watumishi.

matukio katika picha;

Leave a Comment