×

Marekani Yajitoa Rasmi WHO

RAIS  Donald Trump wa Marekani ameliarifu Bunge kuwa Marekani imejitoa rasmi kwenye Shirika la Afya Duniani (WHO).

 

Hatua hiyo imekuja baada ya Trump na serikali yake kuilaani WHO kwa miezi kadhaa na kutishia kukata uhusiano na shirika hilo.

 

Wataalamu na wanachama wa Democrats waliikosoa serikali ya Trump kuwa inajaribu kuhamisha lawama za kushindwa kuitikia ipasavyo janga la virusi vya Corona, na hatua hiyo itatoa athari hasi kwa Marekani kukabiliana na msukosuko huo wa afya ya umma, ambao mpaka sasa umesababisha vifo vya watu zaidi ya laki 1.3 nchini humo.

Leave a Comment