
Benki ya NIC na CBA zimeungana na kuunda benki ya pamoja iitwayo NCBA ambayo itakuwa na nguvu ya kuboresha zaidi masrahi ya wateja wao. Muunganiko huo ulitangazwa jana Jumatano kwenye hafla iliyofanyika Kempinsk Hotel jijini Dar ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt. Bernard Kibesse ambapo ilizinduliwa nembo ya umoja huo.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo mpya (NCBA) Margaret Karume amesema umoja huo hautaathiri wateja waliokuwa katika benki hizo mbili bali utawanufaisha zaidi.

Karume amewaomba wananchi kujiunga na benki hiyo ambayo kwa hapa nchini ina matawi Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Zanzibar ambapo nje ya nchi ina matawi nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Ivory Coast.
Naibu Gavana Dkt. Kibesse amesema kwa upande wake ameridhia na kuudhinisha muungano huo baada ya kuupitia kiumakini na kujiridhisha na mambo mbalimbali ikiwemo kutoathiri masrahi ya wateja.



(HABARI/PICHA:MWANDISHI WETU)