×

Mwili wa Balozi Lusinde Wawasili Dodoma – Video

MWILI wa aliyewahi kuwa waziri katika Baraza la Mawziri la awamu ya kwanza, Balozi Job Lusinde umewasili Dodoma jana ukitokea katika Hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam ambako alifariki.

 

Mdogo wa marehemu ambaye pia ni Waziri Mkuu Msitaafu, mzee Samwel Malechela aelezea taratibu za maziko na kuwashukuru Watanzania wote kwa salam za pole wanazoendelea kuzitoa kwa familia hiyo.

 

Balozi Lusinde (90) ambaye alikuwa mmoja wa baraza la kwanza la mawaziri la Mwalimu Julius Nyerere baada ya uhuru, alifariki dunia alfajiri ya juzi Jumanne, Julai 7, 2020, katika Hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.

 

Lusinde aliyezaliwa Oktoba 9, 1930, aliwahi kuwa Waziri wa Mawasiliano mwaka 1965 na ni miongoni mwa watu waliofanya kazi kwa ukaribu na Mwalimu Julius Nyerere kama Waziri wa Serikali za Mitaa mwaka 1961. Pia, aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini China kuanzia mwaka 1975 hadi mwaka 1984.

 

Leave a Comment