×

Top 5 Wasanii Wenye Albamu Nyingi Bongo

KATIKA mafanikio ya kukuza kazi za msanii na kujivunia, kimoja wapo ni kuwa na album.  Album imekuwa ni kama utambulisho wa msanii katika kazi zake. Kwa zamani album zilikuwa zikifanya poa kiasi kwamba, kuwafanya wasanii kutoa sana album kuliko single.

 

Japo kwa sasa soko la album limeshuka, ila wapo wanamuziki ambao wanaongoza kuwa na album nyingi katika soko la muziki hapa Bongo.

 

MR.2 AMA SUGU

Jina halisi ni Joseph Mbilinyi almaarufu kama Mr. 2 ama Sugu. Ni miongoni mwa waanzilishi wa awali kabisa wa Hip Hop hapa Bongo.

 

Sugu alitamba sana na ngoma yake iliyokwenda kwa jina la Wananiita Sugu. Ni msanii wa kwanza mwenye album kumi katika soko la muziki hapa Bongo, album kama Ni Mimi ya mwaka 1995, Ndani ya Bongo ya mwaka 1996, Niite Mr. 2 ya mwaka 1998, Nje ya Bongo ya mwaka 1999, Millenia ya mwaka 2000, Muziki na Maisha ya mwaka 2001, Itikadi ya mwaka 2002, Sugu ya mwaka 2004, Coming Of Age ya mwaka 2006, VETO ya mwaka 2009 na Antivirus Mixtapes.

Sugu kwa sasa ni mwanasiasa na mbunge wa Mbeya mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

PROFESA JAY

Joseph Haule ‘Profesa Jay’ ni mwanamuziki katika kiwanda cha Hip Hop, ambaye alikuwa msanii aliyewateka mpaka wazee kusikiliza muziki.

Alitamba sana na ngoma ya Zubeda ambayo ilifanya poa sana kwa miaka ya nyuma.

 

Profesa Jay anaongoza kuwa na album sita ikiwemo Machozi, Jasho na Damu ya mwaka 2001, Mapinduzi Halisi ya mwaka 2003, Joseph ya mwaka 2006, Aluta Continua 2007, Izack Mangesho ya mwaka 2014 na Kazi Kazi ya mwaka 2016.

Profesa Jay bado anafanya poa katika muziki na kwa sasa kajikita zaidi kwenye siasa, kwani ni Mbunge wa Jimbo la Mikumi Morogoro kupitia Chadema.

 

LADY JAYDEE

Malkia wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee, alitamba na ngoma ya Machozi. Alibebea heshima katika medani ya muziki kunako mwaka wa 2000 baada ya kutoa albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la Machozi na kutoa single kadhaa kutoka katika albam hiyo na kumfanya kuwa mwanamama wa kwanza katika Bongo Fleva kutumia gharama kubwa ya kuandaa album katika historia ya Bongo Fleva.

 

Album zingine ni kama Binti ya mwaka 2003, Moto (2005), Shukrani (2007), The Best of Lady Jay Dee ya (2012), Nothing But The Truth (2013) na Woman (2017).

Mbali na ukongwe katika gemu la muziki, bado Lady Jaydee anafanya poa kwani ameshiriki katika ngoma mpya ya Harmonize inayokwenda kwa jina la Wife na inafanya poa sana YouTube.

 

RAY C

Muite kiuno bila mfupa Ray C, jina halisi ni Rehema Chalamila, ni mmoja kati ya wasanii wa kike waliotikisa sana miaka ya 2000.

Mnamo mwaka 2003 alitoa album yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la Mapenzi Yangu.

Alianza kujulikana baada ya kutoa vibao kadhaa kama vile; Sikuhitaji, Mapenzi Yangu, Nawewe, Milele, Ulinikataa na nyingine nyingi zilizompa umaarufu.

Album zake nyingine ni kama Na wewe Milele ya mwaka 2004, Sogea Sogea (2006) na Touch Me (2008).

 

JUMA NATURE

Juma Kassim Kiroboto ‘Juma Nature’, ni memba wa kundi la muziki la Wanaume Halisi lililo na maskani yake Temeke, Dar.

Alifanikiwa kutoa album nne, nazo ni Nini Chanzo ya mwaka 2001, Ugali (2003), Ubinadamu Kazi (2005) na Zote History (2006).

 

HAPPYNESS MASUNGA

Leave a Comment