
MSEFMAJI wa Klabu ya Soka ya Simba, Haji Manara, ametoa kiasi cha fedha Tsh 40,000 kwa shabiki wa Yanga, Nyambese Mwita Wambura maarufu kwa jina la Kigelegele; ni baada ya kuwafunga magoli 4-1 katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Azam SportS Federation Cup huku akitoa Tsh 10,000 kwa shabiki wa Simba kwa kufungwa goli moja.

Manara ametoa kitita hicho wakati wa hafla ya kumkabidhi mshindi wa gari mpya aina ya Toyota FunCargo kutoka promosheni ya #ChomokaNaGari2020 #BabaLao, Didas Marik Munishi, wa jijini Dar es Salaam leo Jumatano, Julai 15, 2020, katika ofisi za Global Group zilizopo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.

Promosheni ya Chomoka na Gari ilikuwa ikiendeshwa tangu Februari. 27, 2020, kupitia magazeti bora na yanayoongoza kwa habari za michezo nchini, #Championi & #SpotiXtra.