
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) linapenda kukanusha taaarifa kuwa Mtangazaji Enock Bigwane amepata ajali na kuwa anapatiwa matibabu.
Kumekuwepo na taarifa zikisambaa kuwa Bigwane anapatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa katika ajali ya gari alipokuwa katika mchakato wa kuwania kuteuliwa kugombea Ubunge.
Taarifa sahihi ni kuwa Bigwane hakuwemo ndani ya gari wakati ajali inatokea, lakini ni kweli kuwa ajali ilitokea na dereva wa gari ambaye alikuwa mpambe wake alipoteza maisha (Mungu ampumzishe salama).
Bigwane ni mzima wa afya na tunauomba umma upuuze taarifa zinazoeleza vinginevyo.