×

JPM: Tanzania Iko Salama, Watalii Wanamiminika – Video

RAIS John Magufuli, amesema kuwa Tanzania imebaki kuwa nchi salama  kwa kuwa ilifanikiwa kutokomeza  maambukizi ya ugonjwa wa Covid19 baada ya kumtanguliza Mungu na ndiyo maana hata watalii wameendelea kumiminika nchini kwa kuwa wanao uhakika na usalama wa maisha yao.

 

Ametoa kauli hiyo hii leo Julai 20, 2020, wakati akizungumza na viongozi aliowateua  baada ya kula viapo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

 

“Wizara ya Maliasili nimeanza kuona watalii wengi wanakuja, kuna ndege zinaleta watalii wengi na watu wameangalia na wameuona ukweli kwamba hapa Tanzania tuko salama, maadui zetu watazungumza mengi.

 

“Hata hapa tungekuwa tumevaa barakoa, lakini hakuna aliyevaa.  Hapa ni kwa sababu tuko salama kwani sisi hatuogopi kufa? Lakini Corona iko mbali huko, tuliamua kumuomba Mungu na akatusikia,” amesema.

 

Leave a Comment