
NYOTA wa Filamu Bongo, Jacqueline Wolper ni kama kapagawa na uhusiano wake mpya wa kimapenzi na Rich Mitindo, ambapo anajiweka sawa kumzalia mtoto mahabuba wake ili kuuwekea alama uhusiano wake huo.
Wolper aliliambia Amani Mtandaoni hivi karibuni kuwa umri wake umesogea na kwamba hana cha kusubiri kuzaa na zawadi ya kuwa baba wa mtoto wake anaitoa kwa Rich.“Kwa kweli huu ndiyo wakati wangu na huyu ndiyo baba sahihi kwa mtoto wangu ajaye.

“Nimeridhika naye tangu nilipomuona na jinsi ninavyomjua, heshima hii nampa mpenzi wangu Rich,” alisema Wolper.
STORI: IMELDA MTEMA