
MIMBA ya rapa mkali wa Marekani, Onika Tanya Maraj ‘Nick Minaj’ inadaiwa kumchoma rapa mwenzake, Meek Mill ambaye alikuwa mpenzi wake wa kitambo.
Minaj aliposti picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akionesha mimba hiyo ambayo ni ya mumewe, Kenneth Petty, jambo ambalo liliwafurahisha mashabiki wengi, lakini ikawa tofauti kwa Meek.
Meek aliachia posti moja inayosema; “Unapata muda wa kuposti picha ya Nick akiwa na ujauzito kwenye ukurasa wako, hakujui wala hajawahi kukuposti wewe ukiwa na ujauzito…’’ Akamalizia kwa kucheka.
Ujumbe huo ulitafsiriwa kuwa jamaa huyo alikuwa anaumizwa na mimba ya Minaj.
STORI: PHILADELPHIA, MAREKANI