
MUUZA Magazeti’Venda’ Adam Nuluva amejinyakulia baiskeli baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kwenye shindano lililoandaliwa na kampuni ya Global Publishers kupitia magazeti namba moja ya Michezo Tanzania Champion na Spoti Xtra.
Kampuni hiyo inayochapisha pia magazeti pendewa ya Uwazi, ljumaa, Risasa na ljumaa Wikienda ilianzisha shindano la kuwasaka wauza magazeti bora wa Mkoa wa Morogogo.

Katika shindano hilo endelevu kwa wiki hii wauza magazeti 10 wameibuka washindi na kujinyakulia zawadi mbalimbali huku mshindi wa kwanza, Nuluva aliyeongoza kwa kuuza magazeti mengi ya Global kwa wiki iliyopita, amezawadiwa zawadi ya baiskeli yenye dhamani ya shilingi 115.000 huku mshindi wa pili mpaka wa 10 kila mmoja akikabidhiwa zawadi ya chupa mpya ya chai na T-Shirt za Championi na Spoti Xtra.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa baskeli hiyo na Wakala wa Global Mkoa wa Morogoro Bi. Fatuma Mwigala. Nuluva alisema:

“Awali namshukuru Mungu kuniwezesha kupata zawadi hii ya baiskeli pili naushukuru uongozi wa Kampuni ya Global kwa kutukumbuka sisi wauza magazeti baada ya kuanzisha shindano hili. Baiskeli hii itanisaidi kuzunguka maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Morogoro kuuza magazeti ya Global sambamba na kunisaidia kusambaza kwa haraka magazeti ya oda kwenye maofisi mbalimbali,” alisema Nuluva ambaye anafanya biashara yake ya kuuza magazeti stendi kuu ya mabasi ya mikoani na Msamvu.
Aidha mshindi wa pili mpaka wa tatu Hawa, Bendera, Hamis Shabani’Kiduku’ na Hussein Yahaya Jangama kwa pamoja waliishukuru Kampuni ya Global kwa kuandaa shindano hilo litakalochochea kuwaongezea kasi ya kuuza magazeti ya kampuni hiyo kwa lengo la kupata zawadi kubwa ya baiskeli.
Kwa upande wake wakala wa kampuni hiyo mkoani hapa, Fatuma Mwigala, aliwataka wauza magazeti wa mkoa wa Morogoro kuongeza kasi ya kuuza magazeti ya Global kwa lengo la kuibuka washindi kwenye shindano hilo.
“Kuanzia wiki ijayo shindano hili litaboreshwa zaidi, hivyo na washidi muongeze juhudi kuuza magazeti ya Championi na Spoti Xtra,” alisema
Na Mwandishi Wetu Morogoro.