
WINGA mpya wa Bayern Munich, Leroy Sane, amesema anafurahia kuwa ndani ya kikosi hicho ambacho tayari anaendelea na mazoezi.
Sane alijiunga na Bayern hivi karibuni akitokea Manchenster City na kupewa mkataba wa miaka mitano.
Kwa sasa Bayern inajiandaa kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora dhidi ya Chelsea.
Baada ya kutua hapo, winga huyo amekabi-dhiwa jezi namba 10 ambayo aliiacha mkongwe Arjen Rob-ben na msimu huu im-evaliwa na Philippe Coutinho ambaye ana-kipiga hapo kwa mkopo akitokea Barcelona.
“Nina furaha kuwa hapa, nina furaha zaidi kurejea uwanjani na kufanya mazoezi na timu yangu mpya, hakika ni jambo zuri kwangu,” alisema Sane.
Sane kabla ya kutua Bayern, msimu huu ndani ya Manchester City alicheza mechi moja ya Ngao ya Jamii dhidi ya Liverpool, akaumia dakika za mwanzoni tu, hivyo akawa nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Ikumbukwe Sane sio mgeni wa Bundesliga kwani kabla ya kutua Manchester City, alikuwa akiichezea Schalke kati ya mwaka 2014 na 2016, alifunga mabao 13 na asisti nane katika mechi 57.