×

Video: Binti Mwenye ‘Division One’ Aomba Msaada Wa Kusomeshwa

Irene John ni binti mwenye uwezo mkubwa wa kimasomo ambapo ameweza kufaulu vizuri masomo yake ya sayansi na kupata daraja la kwanza lakini changamoto imekuwa ada ya kuweza kuendelea na kidato cha tano.

 

Hamjui baba mzazi kwani alimtelekeza tangu akiwa mdogo na hajawai kuona mchango wa baba yake huyo kwenye masomo yake na mama yake mzazi ambaye ndiye anakaa naye ana matatizo ya macho yanayompelekea kuona kwa shida sana.

 

Irene hitaji lake ni kuweza kuendelea na masomo yake ya kidato cha tano na kisha cha sita na kisha kubobea kwenye udaktari ambayo ndiyo ndoto yake hivyo anaomba msaada kwa yeyote atakaye guswa aweze kumsaidia angalau apate ada atimize ndoto zake. ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave a Comment