
KOCHA Mkuu wa Klabu ya Namungo, Hitimana Thiery amesema yuko tayari kutua kuifundisha Yanga huku kocha mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji Luc Eymael akisema jamaa ni bonge la kocha.
Hitimana amekuwa akiripotiwa kutakiwa na Yanga ili akawe msaidizi wa Eymael hiyo ni baada ya kutoiva na msaidizi wake wa sasa, Boniface Mkwasa na kocha wa makipa, Manyika Peter.
Hitimana ameliambia Championi Jumamosi kuwa, ni kweli Yanga wanataka akafanye kazi na kocha Eymael, jambo ambalo kwake ameona siyo mbaya kwa kuwa Yanga ni klabu kubwa.
Kocha huyo alisema kwa sasa YALE mashindano makubwa ya wazi ya mchezo wa gofu hapa nchini ya Morogoro Open yaliyopangwa kufanyika mwezi huu, hadi sasa hayajajulikana ni lini yataunguruma huku waandaaji wakitoa sababu inayoendelea kuwaweka kimya.
Ikumbukwe kuwa, awali mashindano hayo yalipangwa kufanyika Julai 18, mwaka huu ambapo, kabla ya tarehe hiyo kufika wahusika walitangaza anasubiri kwanza amalize mchezo wa fainali ya FA ambapo watacheza na Simba Agosti 2, mwaka huu na baada ya hapo ataweka wazi zaidi juu ya mpango huo.
“Ni kweli Yanga wameonyesha kunihitaji, hasa kocha wao ambaye amekuwa akinipigia mara kwa mara akihitaji nikafanye naye kazi.
Kwangu nimeona siyo jambo baya sana kwa sababu Yanga ni timu kubwa na naweza kufanya nao kazi,” alisema Hitimana.
Kwa upande wa Eymael alipoulizwa kuhusiana na mpango huo wa kufanya kazi na Hitimana alisema: “Ni kweli ni kocha mzuri sana, ameonyesha uwezo kwenye ligi ya hapa, namfahamu tangu akiwa Rwanda, kweli natamani kufanya naye kazi, ila uongozi utajua la kufanya.
Stori: Issa Liponda, Dar es salaam