×

Majaliwa Aelekeza Kumuaga Mkapa Kesho – Video

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ametoa melekezo ya shughuli ya kitaifa ya kuaga mwili wa Rais wa Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa katika Uwanja wa uhuru jijini Dar es Salaam itakayofanyika kesho, Julai 28, 2020, kabla ya kwenda kuzikwa kwao, Lupaso Masasi keshokutwa.

 

“Tumeona idadi kubwa ya Watanzania wamekuja hapa kumuaga, pamoja na viongozi mbalimbali ambao wamekuja kumuaga kiongozi wetu, tushukuru Watanzania kwa namna ambavyo wamejitokeza kwa wingi kuja kumuaga.

 

“Kesho watakaopata nafasi ya kuaga ni viongozi wa juu akiwemo Rais, Makamu wa Rais, na Rais wa Zanzibar wataungana na viongozi wa dini na tunaendelea kupata wageni kutoka nchi jirani na wale wote ambao wataingia kesho wataambatana na Mheshimiwa Rais.

 

“Tumenufaika na kazi zake ambazo alizitenda vizuri, amejenga misingi ya utoaji wa huduma kwa Watanzania, tuendelee kumuenzi kila mmoja kwa nafasi yake, sisi Watanzania kwa kweli tupo katika majonzi mazito,” amesema.

 

Wakati huohuo,  Waziri Mkuu wa Burundi, Jen Alain  Bunyoni, amekuwa kiongozi wa kwanza kuwasili nchini kwa ajili ya kuhudhuria shughuli ya kuaga mwili wa hayati Mkapa hapo kesho na kusema kuwa Burundi imepokea kwa mshtuko na majonzi makubwa taarifa za kifo chake.

 

Leave a Comment