Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema litamchukulia hatua za Kinidhamu Kocha Mkuu wa Yanga Sc, Luc Eymael. Kocha huyo ambaye ni raia wa Ubelgiji anadaiwa kutoa matamshi ya kibaguzi hapo jana.
Uongozi wa Yanga umeomba radhi kwa mashabiki wa Yanga viongozi wa shirikisho la mpira nchini Tanzania pamoja na wadau wote wa soka. Yanga imemaliza ligi ikiwa nafasi ya pili baada ya kukusanya alama 72.
Kauli alizozitoa Kocha wa Yanga, Luc Eymael Jana Jumamosi na kupelekea kufukuzwa kazi; “Sifurahii nchi hii [Tanzania]. Nyinyi ni watu ambao hamjaelimika. Nimechukizwa. Sina gari, WiFi au DSTV. Mashabiki hawajui chochote kuhusu Soka. Ni kama nyani au mbwa wanavyopiga kelele.”
